Poem: Maisha Ya Hawker

Hamsini, fifty
Fifty, hamsini
Hamsini, fifty
Ya jioni
Hamsini
Tops
Fifty
Mali
Ya jioni
Fifty, hamsini

Mathee, auntie, sistee
Bei ni ya jioni
Ni kuoya kuoya
Kira kitu na hamsini
Vitu ni ya kamera
Nguo ni ya wanga bado inanuka mafuta ya dege

Ngai Karanja!
Shukua mari haraka
Ndio hao
Kaju na mikebe yao ya miguu ine
Dakika na nusu niko kwa chochoro
Gunia kwa mgongo
Mtoto kwa matiti
Wemeeda!

Ten bob, ashu
Ashu, ten bob,
Maembe, ten bob

Wuu, Mwathani!
Ngati tena diyo hiyo
Giza ya moshi, saa sita mchana
Utadhani al qaeda wamerudi Nairobi
Mguu saidia mimi
Kaatoni na maare nimeshikiria
mbio kama swara
Simba marara, ngozi ya kijani kafunguriwa

Hii ngati haitaki tukure
Wanatupa tear gas ni kama wanaripwa
Na ire mshara ya ngiri tatu
Wanaringa na buduki
Hawajui niko na AK
Ni risasi natafuta
Dio kamau aede fengi nayo

Huku maisha ni survival
Nimeria hadi macho yakazoea
Nimebebwa na Kanjuu
Hata sionangi haja ya kuripa rent kwangu

Wewe,
Unakanyaga matunda nakura kwako
Unafikiria sisi sio watu kama wewe
Nyang’au hii, kwani yako tu dio kazi
Mnajifanya hapa ati kukasirika
Ati tumemarisa farada kwani tumeikura
Nairofi niya kira mtu
Maraya na fathita
Mama boga na shokora
Mwisi na msungu
Hata mimi nimetoa taxi

Ebu mwabie anunue hiyo amekanyaga!

Hii mchezo ya paka na panya
Hauishi reo ama kesho
Kwasababu, kama mimi,
Karao na kanju
Rasima wakure.
Hata wakubwa wanakura mahidi
Na wanakunywa mafuta

Na hiyo ni maedereo

N.W
kenyanpoet(at)gmail.com
Feb, 2009
———————————————————
All right Reserved©

About Kenyan Poet

Showcasing the best in Kenyan Arts;Music,writing,Poetry,fine art and art reviews as well as info on emerging art trends. “Art is not about thinking something up. It is the opposite…getting something down.”